Fuatilia kupitia page ya Chiswagala Stories au Blog ya chiswagalastories.blogspot.com CHISWAGALA ACADEMY KOZI: SAUTI YAKO NDANI YA HADITHI Wiki ya 1: TAMBUA MWANZO WAKO Mkufunzi: Rev. Valentino Chiswagala Kila hadithi nzuri ina mwanzo wake. Lakini mwanzo huo mara nyingi haueleweki au huonekana kuwa si muhimu. Hatuwezi kuandika hadithi kamili ya maisha yetu kama hatujui tulikotoka. Katika wiki hii, tunakusaidia kuangalia nyuma kwa macho ya shukrani, hekima, na maono. Mafundisho ya Wiki 1. Mwanzo sio bahati mbaya Umezaliwa katika familia hiyo, kijiji hicho, au mazingira hayo kwa sababu maalum. Hakuna kilichotokea kwa bahati mbaya. Mungu anaanzisha hadithi yetu kwa misingi inayojenga kusudi. 2. Historia yako ni mbegu ya huduma yako Maumivu, changamoto, na ushindi wa maisha yako ya mwanzo ni mbegu zinazoweza kuzaa huduma, kazi au wito wa maisha yako. 3. Tambua "majira" ya maisha yako Mwanzo wako unaweza kuwa ni utoto wa mateso, furaha, au mchanganyiko. Unapojifunza kusoma...
Posts
Showing posts from May, 2025
KOZI:SAUTI YAKO NDANI YA HADITHI
- Get link
- X
- Other Apps
Fuatilia kupitia page ya Chiswagala Stories au Blog ya chiswagalastories.blogspot.com CHISWAGALA ACADEMY Wiki ya 1: TAMBUA MWANZO WAKO Mkufunzi: Rev. Valentino Chiswagala Kila hadithi nzuri ina mwanzo wake. Lakini mwanzo huo mara nyingi haueleweki au huonekana kuwa si muhimu. Hatuwezi kuandika hadithi kamili ya maisha yetu kama hatujui tulikotoka. Katika wiki hii, tunakusaidia kuangalia nyuma kwa macho ya shukrani, hekima, na maono. Mafundisho ya Wiki 1. Mwanzo sio bahati mbaya Umezaliwa katika familia hiyo, kijiji hicho, au mazingira hayo kwa sababu maalum. Hakuna kilichotokea kwa bahati mbaya. Mungu anaanzisha hadithi yetu kwa misingi inayojenga kusudi. 2. Historia yako ni mbegu ya huduma yako Maumivu, changamoto, na ushindi wa maisha yako ya mwanzo ni mbegu zinazoweza kuzaa huduma, kazi au wito wa maisha yako. 3. Tambua "majira" ya maisha yako Mwanzo wako unaweza kuwa ni utoto wa mateso, furaha, au mchanganyiko. Unapojifunza kusoma majira haya, unaelewa kusudi lak...
KOZI YA MTANDAONI
- Get link
- X
- Other Apps
CHISWAGALA ACADEMY: Kozi ya Mtandaoni kwa Njia ya Maandishi Jina la Kozi: SAUTI YAKO NDANI YA HADITHI – Njia 7 za Kuishi Maisha Yenye Kusudi MKUFUNZI WA KOZI: Rev. Valentino Chiswagala Mwandishi, Mchungaji, na Mhamasishaji wa Kusudi la Maisha Mwanzilishi wa Chiswagala Academy na Chiswagala Stories LENGO KUU LA KOZI: Kumsaidia mshiriki kutambua hadithi yake ya kipekee, kuiponya, kuielewa, na kuitumia kama daraja la utumishi, mafanikio, na ushawishi duniani. MUUNDO WA KOZI: Kozi ya wiki 7 Kila wiki utapokea: PDF ya somo la wiki hiyo Mazoezi ya kujitafakari binafsi Maswali ya kujitathmini Sala au tafakari ya wiki Majadiliano kupitia Telegram/WhatsApp Group (hiari) MADA KUU ZA KOZI (Wiki kwa Wiki): 1. Tambua Mwanzo Wako 2. Maumivu Yako ni Njia ya Mafanikio 3. Kipawa Kilichojificha Ndani Yako 4. Kusikia Sauti ya Ndani – Na Ya Mungu 5. Kikwazo Sio Mwisho 6. Watu Sahihi, Mahali Sahihi 7. Hadithi Yako ni Huduma BONASI ZA KOZI: Ebook ya "Sauti Ndani ya Hadithi...